Isaiah 41:24-29

24 aLakini ninyi ni zaidi ya bure kabisa,
na kazi zenu hazifai kitu kabisa;
yeye awachaguaye ni chukizo sana.

25 b“Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini,
naye yuaja, mmoja toka mawio ya jua aliitaye Jina langu.
Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope,
kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia.
26 cNi nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua,
au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa sawa’?
Hakuna aliyenena hili,
hakuna aliyetangulia kusema hili,
hakuna yeyote aliyesikia maneno kutoka kwenu.
27 dNilikuwa wa kwanza kumwambia Sayuni,
‘Tazama, wako hapa!’
Nilimpa Yerusalemu mjumbe wa habari njema.
28 eNinatazama, lakini hakuna yeyote:
hakuna yeyote miongoni mwao awezaye kutoa shauri,
hakuna yeyote wa kutoa jibu wakati ninapowauliza.
29 fTazama, wote ni ubatili!
Matendo yao ni bure;
vinyago vyao ni upepo mtupu na machafuko.
Copyright information for SwhNEN